Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Fifa kutumia maroboti Kombe la Dunia

Robot Referees And Linesman Roboti

Fri, 10 Jun 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Shirikisho la Soka Kimataifa (FIFA) lipo kwenye mkakati wa kutambulisha maroboti watakaokuwa waamuzi wa pembeni katika michuano ya Kombe la Dunia itakayofanyika Qatar, Novemba mwaka huu.

Rais wa Shirikisho hilo Gianni Infantino imepania kutambulisha mfumo huo wa maroboti kuchezesha mechi za michuano hiyo badala ya marefa wa pembeni.

Majarabio ya mfumo huo yataanza kufanyika katika uwanja uliochezwa fainali ya Kombe la Dunia kwa ngazi ya klabu mwaka jana kabla ya kutambulishwa kwa mashabiki.

Mkutano wa viongozi wa wa FIFA kuhusu hiuo mfumo ulitakiwa kufanyika Qatar tangu Machi mwaka huu, hata hivyo ilipigwa kalenda baada ya vita kati ya Urusi na Ukraine kutibua mipango.

Kwa mujibu wa taarifa FIFA ipo tayari kuanzisha mfumo huo wa maroboti endapo viongozi wengine wataridhishwa kabla ya kuuzindua.

Endapo FIFA itapitisha mfumo huo itakuwa mara ya kwanza michuano ya Kombe la Dunia kuchezwa na maroboti katika historia ya soka.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live