Ferran Torres amemtaarifu bosi wake Pep Guardiola kuwa hamu yake kwa sasa ni kutaka kuondoka Manchester City, huku kukiwa na klabu ya kutokea nchini Hispania kutaka huduma yake.
Wiki iliyopita kulikuwa na tetesi kuwa klabu ya Barcelona ilikuwa inafanya mazungumzo na klabu ya Manchester City ili kuweza kupata huduma ya winga Raheem Sterling lakini mambo yamebadilika baada ya jina la Ferran Torres kuibuka ghafla.
Zimeibuka tetesi kuwa klabu ya Barcelona wamewasilina tena na klabu ya Man City na sasa sio tena Sterling ni Ferran Torres ambaye ameonekana kuvutiwa pia kuhitaji kuhama klabu hiyo.
Mkurugenzi wa michezo wa Barcelona Mateu Alemany ameonekana akifanya vikao kadhaa na viongozi wa klabu ya man city Ferran Soriano, ili kufanikisha uhamisho wa wachezaji hao.