Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Ferran Torres agoma kuondoka Camp Nou

Ferran Torres Camp Nou Ferran Torres

Wed, 19 Jun 2024 Chanzo: Mwanaspoti

Winga wa Barcelona, Ferran Torres ambaye anahusishwa kuwa katika rada za West Ham haitaji kuondoka timu hiyo katika dirisha hili kwani bado anaamini ana nafasi ya kupambania namba katika kikosi cha kwanza cha wababe hao wa Catalonia.

West Ham imepata ujasiri wa kutaka kumsajili baada ya kuona hapati nafasi kubwa ya kucheza na imepanga kumchukua hata kwa mkopo ikiwa itashindikana itamchukua mazima.

BRIGHTON imeanza mazungumzo na wakala wa winga wa Leeds United na Uholanzi, Crysencio Summerville, 22, kwa ajili ya kumsajili katika dirisha hili la majira ya kiangazi.

Summerville ambaye msimu uliopita alicheza mechi 49 za michuano yote na kufunga mabao 21, mkataba wake unatarajiwa kumalizika mwaka 2026 na kuna kila dalili akatua Brighton ambayo imekuwa ikimsaka kwa muda mrefu.

CRYSTAL Palace inataka walau Pauni 65 milioni ili kumuuza beki wao wai kisiki, Marc Guehi anayewindwa na Manchester United dirisha hili.

Guehi ni mmoja kati ya mastaa tegemeo kikosi cha Palace na anavutia timu nyingi kubwa kutokana na kiwango anachoonyesha akiwa na kikosi hicho. Msimu uliopita alicheza mechi 30 za michuano yote. Mkataba wake unamalizika mwaka 2026.

FENERBANHCE tayari imeanza mazungumzo na beki wa Manchester United na Sweden, Victor Lindelof, 29, kwa ajili ya kumsajili katika dirisha hili.

Taarifa kutoka tovuti Sky German zinaeleza kwamba mabosi wa Fenerbahce wameanza mazungumzo ya kumpata Lindelof ikiwa ni moja ya maelekezo ya kocha wao mpya Jose Mourinho. Mkataba wa Lindelof unamalizika mwaka 2025.

ATLETICO Madrid imeanza mazungumzo na Chelsea ili kuipata saini ya kiungo wa timu hiyo, Conor Gallagher, 24, dirisha hili.

Conor ambaye msimu uliomalizika alicheza mechi 51 za michuano yote na kufunga mabao saba, huduma yake pia inawindwa na Tottenham namwenyewe hataki kuondoka kwa sasa kwani anaamini bado ana nafasi ya kupambania namba katika kikosi cha kwanza.

WINGA wa Brazil anayeichezea Palmeiras, Estevao Willian amefaulu vipimo vya afya na kinachosubiriwa ni kusaini mkataba ili kukamilisha usajili wa kujiunga na Chelsea dirisha hili. Estavio, 17, alifikia makubaliano ya kutua Chelsea tangu mwezi uliopita na kilichokuwa kinasubiriwa ni dirisha kufunguliwa ili kukamilisha usajili.

BEKI wa AC Milan na England Fikayo Tomori, 26, hana mpango wa kuachana na timu hiyo katika dirisha hili licha ya Newcastle United kuonyesha nia ya kutaka kumsajili. Tomori ambaye msimu uliomalizika alicheza mechi 35 za michuano yote na kufunga mabao manne, mkataba wake unatarajiwa kumalizika mwaka 2025.

Chanzo: Mwanaspoti