Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Fernando Llorente astaafu Soka

Fernando Llorente Fernando Llorente

Fri, 17 Feb 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mchezaji wa zamani wa Tottenham Fernando Llorente (37), amestaafu soka.

Mshindi huyo wa Kombe la dunia amekuwa bila timu tangu mwishoni mwa msimu uliopita baada ya kuondoka kwenye klabu ya Eibar FC iliyopo kwenye daraja la pili huko Hispania.

Atakumbukwa sana Kaskazini mwa London kwa goli lake lenye utata katika robo fainali ya kishindo kwenye Ligi ya Mabingwa dhidi ya Manchester City mwaka 2019.

Mshambuliaji huyo alishinda Ligi ya Uropa akiwa Sevilla na alikuwa sehemu ya timu za Hispania zilizoshinda Kombe la Dunia 2010 na Euro 2012. Amewahi pia kuchezea Juventus, Swansea.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live