Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Ferguson atoa neno la matumaini United

Fergie X Jeff Ferguson atoa neno la matumaini United

Fri, 24 Nov 2023 Chanzo: Mwanaspoti

Kocha wa zamani wa Manchester United, Sir Alex Ferguson amesema ana matumaini makubwa juu ya tajiri Sir Jim Ratcliffe anayetarajiwa kuwekeza kwenye timu hiyo katika siku za hivi karibuni.

Bilionea huyo anatarajiwa kukamilisha mchakato wa kununua hisa za asilimia 25 kwa Pauni 1.3 bilioni kutoka kwa familia ya Glazer ambayo iligoma kuiuza jumla jumla timu hiyo.

Taarifa za awali zilikuwa zinaeleza kwamba mchakato huo huenda ungekamilika katika mapumziko ya ligi kupisha wiki ya kimataifa ya mwezi huu lakini unaonekana kuchelewa.

Hata hivyo, mara baada ya mchakato kukamilika, makubaliano yaliyofikiwa na pande zote mbili ni kwamba Ratcliffe atakuwa ndio anasimamia masuala yote yanayohusiana na masuala ya mpira wa miguu ndani ya timu hiyo na hivi karibuni iliibuka taarifa kwamba atakuwa akishauriana na Ferguson juu ya nini kifanyike.

“Mimi bado ni mmoja kati ya wakurugenzi wa timu na namfahamu vizuri Jim Ratcliffe, acha tusubiri na tuone nini atafanya lakini mimi nina matumaini makubwa katika ujio wake.”

Mapema wiki hii baada ya kutoka taarifa kwamba Ratcliffe atakuwa akichukua ushauri kutoka kwa Ferguson mwenye umri wa miaka 81, ziliibuka ripoti kuwa kuna uwezekano mkubwa Fougie Freedman akaajiriwa kwenye timu kuwa mkurugenzi wa michezo mpya.

Freedman ambaye ni raia wa Scottland anaifanya kazi kama hiyo akiwa na Crystal Palace na anapewa nafasi kwa sababu ni rafiki wa karibu na Ferguson na aliwahi kuwa jirani yake pia huko Cheshire, jijini Manchester.

Wiki iliyopita mwenyekiti wa Crystal Palace, Steve Parish alisema hadi sasa hakuna mazungumzo yoyote yaliyofanywa baina ya Freedma na Man United kuhusu kumpa ajira lakini inawezekana ikawa asilimia 50 ni ukweli juu ya taarifa hiyo.

Mashabiki wengi wa Man United wamekuwa wakiwapinga wamiliki wa timu hiyo familia ya Glazer na mara kadhaa wameitisha maandamano nje ya uwanja wa Old Trafford wakishinikiza waondoke.

Matajiri wengi walijitokeza kuinunua timu baada ya kutangazwa kwamba inauzwa lakini changamoto ilikuwa ni kwenye makubaliano ya bei na baadhi ya wanafamilia walikuwa hawataki kuona timu hiyo ikiuzwa jumla.

Miongoni mwa matajiri hao alikuwepo Sheikh Jassim Al Thani kutoka Qatar ambaye kwa mujibu wa ripoti alijiondoa katika wiki chache zilizopita baada ya mazungumzo ya muda mrefu.

Man United kwa sasa imekuwa ikipitia wakati mgumu ndani ya uwanja ambapo haijaanza vizuri kwenye Ligi Kuu England kwa msimu huu ikicheza mechi 12 za michuano yote na kukusanya alama 21.

Chanzo: Mwanaspoti