Makocha magwiji wa ligi kuu ya ligi kuu ya Uingereza Sir Alex Ferguson wa Manchester United na Arsene Wenger wa klabu ya Arsenal wamejumuishwa kwenye tuzo ya heshima ya ligi kuu ya kuu Uingereza maarufu kama Premier league Hall of Fame.
Tuzo ya heshima ya ligi kuu ya Uingereza imekua ikijumuisha wachezaji zaidi lakini mwaka huu 2023 ndio imeanza kujumuisha makocha na ndio makocha wawili hao magwiji Sir Alex Ferguson na Arsene Wenger wamejumuishwa katika tuzo hiyo heshima ya ligi kuu ya Uingereza.
FergusonTuzo za Premier League Hall of Fame zimeanza kutolewa mwaka 2021 zikianza kujumuisha wachezaji mbalimbali na tuzo hizo zimelenga kuwapa heshima wachezaji ambao wamecheza kwenye ligi kuu ya Uingereza kwa mafanikio makubwa, Vilevile wachezaji waliocheza kwenye viwango vya juu zaidi kwenye historia ya ligi hiyo.
Kocha Sir Alex Ferguson amefanikiwa kua kocha mwenye mafanikio zaidi kwenye historia ya ligi kuu ya Uingereza, Kwani kocha huyo amefanikiwa kushinda mataji 13 ya ligi kuu ya Uingereza kwa kipindi cha miaka 26 ambacho amekua akihudumu kwenye klabu ya Manchester United.
FergusonKocha Arsene Wenger vilevile amefanikiwa kua kwenye tuzo ya heshima baada ya kudumu kwa muda mrefu ndani ya ligi kuu ya Uingereza akihudumu ndani ya klabu ya Arsenal kwa muda wa miaka 22, Huku akifanikiwa kutwaa mataji matatu ya ligi kuu ya Uingereza hivyo leo amejumuishwa pamoja na Ferguson kwenye tuzo hiyo ya heshima mapema leo.