Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Fergie ahangaika kujata kikosi chake

PA16564407 2947700 Sir. Alex Ferguson

Sun, 9 Jun 2024 Chanzo: Mwanaspoti

Sir Alex Ferguson ametaja staa mmoja tu mwenye uhakika wa kupata namba kwenye kikosi chake bora cha muda wote kwa miaka yote aliyofanya kazi ya kuinoa Manchester United.

Kocha huyo Mskochi, Fergie aliingoa Man United kwa miongo mitatu na kunyakua mataji 13 ya Ligi Kuu England akiwa Old Trafford.

Katika zama zake kwenye klabu hiyo, Fergie aliwanoa mastaa kibao mahiri akiwamo Cristiano Ronaldo, Wayne Rooney, Eric Cantona na Ryan Giggs kwa kuwataja kwa uchache.

Zama zake Old Trafford zilifika mwisho 2013 baada ya kuiongoza Man United kubeba taji la Ligi Kuu England, ambalo ni la mwisho kwao, bado hawajabeba taji jingine la ubingwa huo tangu wakati huo.

Na hapo, kocha huyo aliulizwa kuhusu kikosi chake cha kwanza cha muda wote, ndipo aliposema kwa wachezaji wote aliowahi kuwanoa, ni mmoja tu mwenye uwezo wa kuingia kwenye kikosi cha timu zake zote.

Fergie alisema: “Ukweli, nitasema Denis Irwin ni mtu wa kwanza kwenye timu yangu. Naweza kumjumuisha kwenye timu zangu nane kati ya 10.

“Pale Highbury katika mechi moja hivi, alipiga pasi ya nyuma dakika za mwisho ilinaswa na Dennis Bergkamp na kufunga.

“Baada ya mechi, kwenye kikao cha waandishi niliulizwa, ‘Utakuwa umekasirishwa na ile pasi ya nyuma.’ Nilisema, ‘Hapana, kosa moja kwenye kipindi cha miaka 10 si jambo baya’. Alikuwa mchezaji wa aina yake.’”

Irwin alijiunga na Man United akitokea Oldham, Juni 1990 na kwenda mchezaji muhimu wa kikosi hicho, akishinda mataji 18 katika misimu 12.

Fergie aliendelea: “Ngumu sana. Mfano una idadi ya mastraika niliokuwa nao, kuanzia kwa (Brian) McClair, (Mark) Hughes, (Andy) Cole, Cantona, (Ruud) van Nistelrooy, (Louis) Saha, Ole Gunnar Solskjaer, (Dwight) Yorke, Teddy Sheringham.

“Kisha kuna hawa wachezaji wa sasa Wayne Rooney, (Robin) van Persie, Chicharito (Javier Hernandez). Utamchagua nani hapo? Cantona na mwingine mmoja pengine? Kwenye kiungo kulikuwa na (Roy) Keane, (Bryan) Robson na Scholes -- wote ni wachezaji mahiri --na kuna David Beckham, Ronaldo na Ryan Giggs.”

Chanzo: Mwanaspoti