Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Ferdinand: Chelsea watajuta kumuuza Mount

Mason Mount Move Mason Mount

Mon, 10 Jul 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Gwiji wa Manchester United na England, Rio Ferdinand amesema kuwa kitendo cha Chelsea kukubali kumuuza Mason Mount kwenda United watakuja kukijutia siku za mbeleni.

Rio, ameelezea furaha yake baada ya Manchester United kukamilisha usajili wa Mason Mount kwa pauni milioni 60.

United watalipa pauni milioni 55 pamoja na pauni milioni 5 kama nyongeza kwa Mount ambaye amesaini mkataba hadi Juni 2028 akiwa na chaguo la kuongeza huku akitarajiwa kulipwa mshahara wa pauni 250,000.

Rio alisema, Mount ni mchezaji mzuri ambaye anakwenda kuiongezea kitu United na kwa upande wa Chelsea ni hasara kwa kuwa wameruhusu mchezaji mzuri aondoke.

Mount amepewa jezi namba 7 ambayo inaheshima kubwa sana ndani ya United kwa kuwa wachezaji waliowahi kuivaa jezi hiyo waliacha alama ya kufanya mambo makubwa kama Cristiano Ronaldo.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: