Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Fenerbahce yaicheleweshe Galatasaray Ubingwa

Fene Vs Gala Fenerbahce yaicheleweshe Galatasaray Ubingwa

Wed, 22 May 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Galatasaray walishindwa kutwaa UBINGWA wao wa 24 wa Ligi BAADA ya kupokea kipigo cha goli moja (1) kutoka kwa wapinzani wao wa karibu FENERBAHCE siku ya Jumapili.. FENERBAHCE walicheza pungufu kwa zaidi ya dakika 69' baada ya mchezaji wao Alexander Djiku kuoneshwa kadi nyekundu dakika ya 21' tu ya kipindi cha kwanza.

Hivyo basi Bingwa wa Ligi ya Uturuki atafahamiki michezo ya mwisho itakayopigwa 25/26 May 2024.

Galatasaray watashuka dimbani ugenini kunako dimba la Medas Konya Buyuksehir kupepetana na Konyaspor.

Fenebahce wao watakuwa nyumbani kunako dimba la Ülker kuwakaribisha Istanbulspor..

Galatasaray wapo kileleni na alama zao 99, michezo 37, huku Fenerbahçe wao wakiwa nafasi ya pili na alama zao 96 BAADA ya kucheza michezo 37 pia ..

Chanzo: www.tanzaniaweb.live