Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Feisal mchezaji bora, Nabi kocha bora wa Ligi mwezi Oktoba

Feisal Mchezaji bora wa Mwezi Oktoba, Feisal Salum

Tue, 9 Nov 2021 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kiungo wa Yanga, Feisal Salum ameteuliwa Mchezaji Bora wa mwezi Oktoba wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara huku kocha wake, Mtunisia, Nasreddine Nabi akiteuliwa Kocha Bora wa mwezi huo.

Katika taarifa yake Bodi ya Ligi imesema kwamba mshambuliaji wa Polisi Tanzania, Vitalis Mayanga ameteuliwa Mchezaji Bora wa mwezi wa kwanza wa msimu, Septemba huku kocha wake, Malale Hamsini akiteuliwa Kocha Bora mwezi huo wa tisa.

Tumaini Ikomba ameteuliwa Meneja Bora wa Uwanja mwezi Septemba kwa nzuri Uwanja wa Black Rhino uliopo Karatu na Modestus Mwaluka amekuwa Meneja Bora wa Oktoba kwa kazi yake nzuri Uwanja wa Sokoine uliopo Mbeya.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live