Mabingwa watetezi wa Ligi Kuu Tanzania Bara, Timu ya Yanga imekwea kileleni mwa msimamo wa Ligi baada ya kuichapa KMC bao 1-0 mchezo uliopigwa leo Oktoba 26 katika Uwanja wa Benjamin Mkapa.
Yanga ambao walikuwa na mabadiliko makubwa katika kikosi chao cha leo, walianza mchezo kwa kasi ndogo pengine ni kutokana na kuwakosa nyota wao kadhaa wa kikosi cha kwanza kama Kiungo Khalid Aucho, Fiston Mayele, Kibwana Shomari, Djuma Shaban huku wachezaji kama Feisal Salum, Jesus Moloko wakianzia benchi.
Mpaka mchezo unakwenda mapumziko hakuna timu iliyofanikiwa kuona lango la mwenzake huku KMC wakionekana kutawala sehemu kubwa ya mchezo katika dakika 45 za kipindi cha kwanza.
Kipindi cha pili Yanga ilifanya mabadiliko ya kuwatoa Bakari Mwamnyeto, Tuisila Kisinda na Dickson Ambundo huku wakiingia Feisal Salum, Jesus Moloko na Zawadi Mauya.
Mabadiliko hayo yalimfanya Bangala ambaye alianza kama kiungo arudi kwenye beki wa kati kucheza sambamba na Ibrahim Bacca.
Wakati huo huo Aziz Ki ambaye alianza kama mshambuliaji wa pili alienda kucheza winga ya kulia aliyokuwa anacheza Kisinda ma eneo la ushambuliaji alienda kucheza Feisal Salum.
Mabadiliko hayo yaliifanya Yanga ipeleke mashambulizi kwa spidi langoni kwa KMC tofauti na ilivyokuwa kipindi cha kwanza.
Dakika ya 55 Yanga ilitaka kupata bao la kuongoza baada ya Jesus Moloko kupiga shuti la juu juu lakini kipa David Kissu aliucheza na kuwa kon ma isiyokuw na faida.
Wakati huohuo Kelvin Kijiri alionyeshewa kadi ya njano baada ya muamuzi Hery Sasii kuonyesha amemfanyia madhambi Farid Mussa na kipa wao Kissu alionyeshewa kadi ya njano bada ya kuonekana anapoteza muda.
Dakika ya 59 Bigirimana wa Yanga alionyeshewa kadi ya njano baada ya kumfanyia madhambi Hance Masoud.
Mchezo kwenye kipindi cha pili uligeuka kucheza kwa kukamiana kwani walikuwa hawapeani nafasi kubwa ya kucheza.
Dakika ya 66 KMC nayo ilifanya mabadiliko ya kuwatoa Awesu Awesu Emmanuel Mvuyekure na nafasi zao waliingia Masoud Abdalah (Kabaye) na Daruesh Saliboko.
Mshambuliaji wa KMC, Matheo Anthony alikosa utulivu dakika ya 69 kuiandikia bao timu yake baada ya Makang’a kuoiga krosi na yeye kuubutua mpira ukienda nje.
Yanga ilijibu shambulizi dakika ya 74 baada ya Gael Bigirimana kupiga krosi na Makambo aliiunga kwa kichwa mpira ukagonga mwamba na mabeki wa KKMC wakauondoa.
KMC nayo ilijibu mapigo baada ya Daruesh Saliboko kumpigia pasi Matheo Anthony ambaye alifyatuka shuti lililoishiw mikononi mwa kipa Diara Djigui.
Yanga ilionyesha kuhitaji ushindi kwani dakika ya 78 ilimtoa Bigirimana na kuingia Denis Nkane, mabadiliko hayo yakimrejesha Feisal kwenye kiungo na Nkane kucheza ushambuliaji.
Dakika ya 80 Yanga ilipata bao la kuongoza baada ya kutokea piga nikupige langoni kwa KMC na Feisal alipiga mpira na kwenda wavuni.
Dakika ya 85 KMC iliwatoa Kelvin Kijiri na Styve Nzigamasabo na kuingia Boniphace Maganga na Waziri Junior.