Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Feisal: Sishindani na yoyote Ligi Kuu

WhatsApp Image 2024 05 09 At 10.52.31.jpeg Feisal: Sishindani na yoyote Ligi Kuu

Thu, 9 May 2024 Chanzo: dar24

Kiungo kutoka visiwani Zanzibar na Klabu ya Azam FC, Feisal Salum ‘Fei Toto’ amesema kila anachokifanya uwanjani ni kwa ajili ya timu yake na anapofunga hakuna anayeshindana naye, bali ni kuipa matokeo mazuri timu yake.

Nyota huyo amesema anafurahi kuona anaisaidia zaidi timu yake kuweza kupata matokeo mazuri katika kila mchezo.

Azam FC leo Alhamis (Mei 09) inashuka uwanjani kuumana na Simba SC kwenye mfululizo wa michezo ya Ligi Kuu Tanzania Bara inayokwenda ukingoni.

“Kila ninachokifanya uwanjani ni kwa ajili ya timu yangu, sichezi kwa kushindana na mtu, nacheza kuisaidia timu kufanya vizuri, nashukuru Mungu kwa kila kitu kizuri ninachokifanya kwa ajili ya timu, ushindi tunaopata niwe nimefunga mimi au mtu mwingine unatokana na jitihada na juhudi za wachezaji wote,” amesema Fei Toto.

Fei Toto mpaka sasa ameifungia timu yake mabao 15 na kutoa pasi za magoli ‘asisit’ saba akilingana na kiungo wa Young Africans, Azizi Kii.

Mashabiki wa soka nchini tayari wameanza kuwashindanisha nyota hao kutokana na kasi yao ya kufunga huku wakiwa wamelingana idadi ya mabao ya kufunga na wanaamini mfungaji bora msimu huu atatoka kati yao.

Chanzo: dar24