Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Feisal, Mwamnyeto watakata Yanga ikiishushia kipigo Ruvu Shooting

Fei Toto Yanga Ruvu Feisal, Mwamnyeto watakata Yanga ikiishushia kipigo Ruvu Shooting

Tue, 4 Oct 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kiungo fundi wa Yanga, Feisal Salum 'Fei toto' alikua mwiba mkali kwa Ruvu Shooting kwenye mchezo wa Ligi Kuu Bara ambao Wananchi waliibuka na ushindi wa mabao 2-1.

Licha ya Maafande hao kumweka chini ya ulinzi, kinara wa mabao wa Yanga, Fiston Mayele walikiona chamoto kupitia kwa Feisal ambaye alifungua ukurasa wa  mabao kwa vijana hao wa Nasreddine Nabi.

Mbali na bao la kichwa ambalo alifunga Feisal dakika ya 52 baada ya krosi nzuri ya Joyce Lomalisa, alikuwa kiunganishi mzuri kwa Yanga katika kujenga mashambulizi yao.

Feisal alikuwa akishuka chini kuongeza nguvu kwa Yannick Bangala na Abubakar Salum 'Sure Boy' mabao walikuwa wakicheza eneo la kiungo.

Hakuishia hapo wakati mabao mabeki wa Ruvu Shooting walipokuwa wakipambana na Mayele alikuwa akipata nafasi ya kuwa huru kiasi cha kuwafanya Maafande hao kuwa kwenye hatari.

Dakika ya 71, Yanga ilijihakikishia ushindi na kufikisha pointi 13 kupitia kwa Bakari Mamnyeto ambaye alirejea kwa kuanza kwenye kikosi cha kwanza cha Nabi.

Yanga ilifanya mabadiliko kadhaa ikiwemo kuingia kwa Makambo, Dickson Ambundo, Dennis Nkane na Khalid Aucho huku wakitolewa, Mayele, Farid Mussa na Kisinda na Sure Boy.

Ruvu ilipata bao la kufutia machozi kupitia kwa Rollan Msonjo dakika nne kabla ya mchezo huo kumalizia.

Kikosi cha Ruvu Shooting, Hussein Msalanga, Michael Aidan, Mpoki Mwakinyuke, Tariq Abed, Frank Nchimbi,Rolland Msonjo,  Ally Kombo, Shaban Msala, Samsoni Joseph, Rashid Juma na Abalkassim Sulleiman.

Yanga,  Djigui Diarra, Djuma Shabani, Joyce Lomalisa, Bakari Mwamnyeto, Dickson Job, Yanick Bangala, Salumu Abubakar , Feisal Salum,  Farid Mussa, Fiston Mayele na Tuisila Kisinda.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live