Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Feisal, Mudathir wategeana kuingia uwanjani

Fei X Mudathir Feisal, Mudathir wategeana kuingia uwanjani

Mon, 23 Oct 2023 Chanzo: Mwanaspoti

Viungo Feisal Salum wa Azam FC na Mudathir Yahya wa Yanga wamezua kihoja kwenye mchezo ambao umezikutanisha timu zao kwa kutegeana kuingia katika eneo la kuchezea la Uwanja wa Benjamin Mkapa.

Tukio hilo lilitokea wakati vikosi vya timu hizo vikiingia uwanjani hapo tayari kuanza dakika 45 za kipindi cha kwanza ndipo wachezaji hao waliposimama kwenye mstari wa kuingia eneo la kuchezea.

Wakati wachezaji wenzeo wakijipanga na kusalimiana, Feisal na Mudathir waliendelea kutegeana hadi zoezi hilo lilipokamilika huku kila kikosi kikienda upande wake.

Wakati taharuki kwa mashabiki ikiwa kubwa baada ya kustukia kitendo hicho, ndipo Mudathir alipoamua kuwa wa kwanza kwenda kuungana na wenzake huku Feisal naye akifuata na kupiga picha za vikosi.

Kwa mujibu wa kanuni za ligi wachezaji hao wanaweza kukumbana na adhabu kwa kitendo hicho ambacho.

Fei Toto azomewa, Bangala apigiwa makofi

Kwenye mchezo wa Ligi kuu Bara unaochezwa katika uwanja wa Benjamin Mkapa kati ya wenyeji Yanga dhidi ya Azam FC, limetokea tukio la kushangaza kwa namna moja ama nyingine.

Azam FC waliitangulia Yanga kuwasili katika uwanjani hapo dakika tano baadae Yanga nao walifika kuashiria mbungi kuchezwa.

Baada timu zote mbili kutokufanya mazoezi ya mwisho katika uwanja wa mechi jana kwakuwa kulikuwa na mchezo wa AFL kati TP Mazembe dhidi ya Espresse de Tunis, leo timu hizo zililazimika kuingia uwanjani kukagua uwanja (pitch feeling).

Azam FC ndio walikuwa wakwanza kukagua uwanja, wakati wao wanatoka Yanga nao walikuwa wakiingia kukagua uwanja na ndipo Feisal Salum pamoja na Yanick Bangala wakakutana na rafiki zao na kusalimiana.

Feisal akiwa anarudi kwenye vyumba vya kubadilishia nguo mashabiki wa Yanga wanaoketi jukwaa la VIP B walionekana kumzomea na yeye hakuonyeaha ishara wala maneno ya kujibu chochote.

Wakati Bangala naye akirudi kwenye vyumba vya kubadilishia nguo mashabiki hao hao walisimama na kumpigia makofi.

Feisal aliondoka Yanga kwa namna mashabiki hawakuridhika nayo akisema kuwa hakuwa na uhusiano mzuri na Rais wa timu hiyo Eng Hersi Said.

Chanzo: Mwanaspoti
Related Articles: