Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Fei toto na unahodha

Nahodha Fei Toto Kiungo wa Yanga Feisal Salum, akiwania mpira na mchezaji wa Geita

Sat, 2 Oct 2021 Chanzo: www.mwanaspoti.co.tz

Kiungo Feisal Salum wa Yanga nyota yake ni kama imeanza kung’aa baada ya kuendelea kupewa kitambaa cha unahodha kwenye mechi ya pili mfululizo.

Feisal alianza kuvaa kitambaa hicho kwenye mchezo uliopita dhidi ya Kagera Sugar ambao alifunga bao la ushindi Yanga wakishinda 1-0.

Kwenye mchezo wa leo dhidi ya Geita Gold, kocha wa Yanga, Nassredine Nabi ameendelea kumpa kitambaa Feisal kama ilivyokuwa kwenye mchezo uliopita.

Kukosekana kwa manahodha Bakari Mwamnyeto na Tonombe Mukoko kwenye kikosi cha Yanga kwasasa kumemfanya Fei apewe kitambaa hicho.

Mchezaji mwingine ambaye huwa anavaa kitambaa hicho ni  Deus Kaseke lakini hajawa mchezaji wa kuanza katika kikosi cha kocha Nassredine Nabi.

Katika msimu uliopita manahodha wa kikosi cha Yanga walikuwa ni Bakari Mwamnyeto, Haruna Niyonzima, Tonombe Mukoko na Deus Kaseke.

Chanzo: www.mwanaspoti.co.tz