Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Fei Toto vs Yanga, mbivu na mbichi kujulikana kesho

Feisal Salum Fei Toto Aongeza Mkataba Yanga Sc Fei Toto vs Yanga, mbivu na mbichi kujulikana kesho

Wed, 1 Mar 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Baada ya Sintofahamu ya muda mrefu kuhusu sakata la mchezaji Feisal Salum 'Fei toto' na klabu ya Yanga, kesho Machi 2, 2022 ndiyo siku yatafanyika mapitio 'review' ya kesi baina ya pande zote hizo mbili pamoja na kamati ya Sheria na hadhi za wachezaji ya Shirikisho la Soka nchini (TFF).

Ikumbukwe Yanga ilipeleka shauri kwenye kamati hiyo ikimtaka Feisal kutoa maelezo kwanini ameondoka ndani ya kikosi hicho na kuandika barua ya kuaga akiichapisha katika ukurasa wake rasmi wa mtandao wa kijamii wa Instagram, Desemba 24,2022 bila mazungumzo ya pande zote mbili.

Baada ya hapo shauri hilo kwa mara ya kwanza lilisikilizwa Ijumaa ya Januari 6 mwaka huu na baada ya hapo TFF ilitoa barua iliyoeleza Fei Toto bado ni mchezaji halali wa Yanga kimkataba na kutoa nafasi ya upande wa mchezaji huyo kuomba mapitio ya shauri hilo kama hawataridhika na maamuzi yaliyotolewa.

Hata hivyo upande wa Fei Toto kupita kwa mawakili wake wakiongozwa na Nduruma Majembe na Makubi Kanju hawakukubaliana na majibu ya TFF na kuomba ‘review’ ambayo hatimaye itasikilizwa kesho.

Kabla ya kesho shauri hilo lilipangwa kusikilizwa February 27, lakini ikasogezwa mbele ambapo itaanza saa 4:00 asubuhi katika ofisi za TFF Karume, Dar es Salaam.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live