Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Fei Toto ni mchezaji bora msimu huu

Fei Toto Azam Mkd Fei Toto ni mchezaji bora msimu huu

Thu, 23 May 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mchambuzi wa masuala ya soka nchini kutoka TV3, Boiboi Mkalai amedai kuwa kiungo mshambuliaji wa Azam Fc, feisal Salum 'FDei Toto' ndiye anafaa kupewa tuzo ya mchezaji bora wa Ligi msimu huu.

Fei Toto amepachika mabao 16 kwenye ligi na assists 7 nyuma ya Aziz Ki mwenye mabao 17 na assists nane mpaka sasa zikiwa zimesalia mechi mbili kutamatika kwa ligi.

"Unaweza ukawa mgumu kuelewa katika hili kwakua utakuwa umepima mafanikio ya Yanga dhidi ya Azam FC.

"Lakini ninachokitazama ni performance ya Azam fc msimu huu na ujio wa Feisal katika kikosi, Mpaka sasa faisali ni kinara wa mabao katika ligi yetu na amefanikisha kuiweka Azam juu ya Simba kwa utofauti wa mabao.

"Watu wanaweza wakaja na jina la Aziz Ki kwakua timu yake ametwaa ubingwa, Lakini Aziz msimu huu kuna baadhi ya mechi alikosekana katika kikosi cha Yanga na Yanga ilikuwa inapata matokeo chanya.

"Unaweza ukajiuliza kama Fei toto kwa bahati mbaya angekumbwa ba majeraha je? Azam FC wangeweza kufikia hapa walipo leo, Hii inamaanisha mchango wa Fei ni mkubwa kwenye timu kuliko Aziz Ki ndani ya Yanga Africa.

"Hivyo kwa ubora na mafanikio binafsi yaliyopelekea timu kuwa bora katika msimu huu yamechangiwa na Feisal Salum (Fei Toto)," amesema Boiboi Mkali.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live