Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Fei Toto mkali ndani ya boksi

Feisal Salum Fei Toto Msamah Kiungo mshambuliaji wa Azam FC, Feisal Salum 'Fei Toto',.

Fri, 3 May 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kiungo mshambuliaji wa Azam FC, Feisal Salum 'Fei Toto', ndiye kinara wa kufunga mabao ndani ya eneo la hatari mpaka kufikia raundi ya 24 ya Ligi Kuu Tanzania Bara inayoelekea ukingoni.

Takwimu za dawati la michezo la Nipashe pamoja na Bodi ya Ligi zilizotolewa jana, Fei Toto amefunga mabao 13 akiwa katika eneo la 18.

Mchezaji huyo aliyesajiliwa msimu huu akitokea Yanga, ana mabao 14 ya kufunga mpaka sasa, hivyo takwimu zinaonyesha ni bao moja tu alilolifunga akiwa nje ya boksi.

Wanaoshika nafasi ya pili kwa kupachika mabao ndani ya boski ni kiungo mshambuliaji wa Yanga, Stephane Aziz Ki na straika wa KMC, Waziri Junior, ambao wote wamefunga magoli 10 wakiwa ndani ya eneo la hatari.

Aziz Ki, ndiye kinara wa ufungaji kwenye ligi mpaka sasa, akiwa na mabao 15, hivyo mabao matano ametafunga akiwa nje ya eneo la hatari na Waziri ana mabao 11, hivyo ni bao moja tu ambalo amelifunga akiwa mbali na lango.

Takwimu zinaonyesha kiungo mwingine wa Yanga, Mkongomani Maxi Nzengeli na straika wa Prisons, Samson Mbangula, wamefunga mabao manane ndani ya boksi kila mmmoja.

Nzengeli amefunga tisa katika Ligi Kuu, hivyo moja amelifunga nje ya boksi, lakini Mbangula ana mabao manane, mabao yote aliyoyafunga, ameyapachika akiwa ndani ya eneo la hatari.

Wachezaji Jean Baleke aliyekuwa akiichezea Simba, Prince Dube wa Azam FC, Pacome Zouzoua na Mudathir Yahya wa Yanga, wote wana mabao saba kila mmoja waliyoyafunga wakiwa ndani ya eneo la hatari.

Takwimu zinaonyesha Baleke na Mudathir ambao kila mmoja ana mabao manane, kila mmoja kati yao amefunga bao moja nje ya boksi, lakini Dube na Pacome mabao yao yote saba wameyapachika wakiwa ndani ya eneo la hatari.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live