Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Fei Toto mguu wake wa bahati huu hapa

Fei Toto 9 Goals Fei Toto mguu wake wa bahati huu hapa

Thu, 6 Jun 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Ingizo jipya ndani ya kikosi cha Azam FC mguu wake wa dhahabu ni ule wa kulia kutokana na kasi yake kuwa katika ubora ndani ya uwanja.

Nyota huyo alikuwa akipambana na mwamba Aziz Ki kwenye kutupia mabao uwanjani na mwisho msimu wa 2023/24 ikajulikana kuwa mkali ni Aziz Ki ambaye alitupia mabao 21 akiwa ni mfungaji bora.

Mguu wa kulia alikuwa bora ambapo katupia jumla ya mabao 13 kati ya 19 ambayo amefunga kiungo huyo wa Azam FC inayonolewa na Kocha Mkuu Yusuph Dabo.

Mwamba Saido Ntibanzokiza katupia mabao 10 kwa mguu wa kulia kati ya 11 ambayo amefunga huku Mudathir Yahya akitupia mabao 9 kwa mguu wa kulia.

Jean Baleke wa Simba katupia mabao 8 kwa mguu wa kulia sawa na Marouf Tchakei wa Ihefu, Reliants Lusajo wa Namungo na Maxi Nzengeli wa Yanga.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live