Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Fei Toto kupigwa bei na Azam FC, bei yaanikwa

Feisal Salum Fei Toto Msamah Fei Toto

Tue, 2 Apr 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Klabu ya Azam, imeweka wazi dau wanalolitaka kwa timu inayohitaji huduma ya kiungo mshambuliaji wao, Feisal Salum ‘Fei Toto’, kuwa ni dola za Kimarekani milioni mbili sawa na Sh. bilioni 5.1 za Tanzania.

Akizungumza nasi jana, Ofisa Habari wa Azam FC, Hashim Ibwe, alisema hawajatangaza kumuuza Fei Toto, lakini kama kuna klabu inamhitaji, italazimika kuvunja mkataba wake kwa kipindi kilichobakiwa, amabao una thamani ya dola za Kimarekani milioni mbili.

Alisema wamekuwa na utamaduni mzuri wa kuwauza wachezaji wao endapo kuna timu inahitaji mchezaji ndani ya klabu yao na wameshafanya hivyo mara kadhaa hapo nyuma.

“Hatujawahi kuwa wachoyo na mtu ambaye ana mhitaji mchezaji hapa Azam FC, kwa sababu tumekuwa na wachezaji na kuwaacha na kwenda katika klabu mbalimbali wakiwamo Aishi (Manula), Kapombe (Shomari), Erasto (Nyoni), Mudathir (Yahya) na Salum Aboubakar.

"Hatujatangaza ofa juu ya Fei Toto bali kama kuna klabu ambayo inamhitaji kiungo huyo tunawakaribisha waje mezani, tumepiga hesabu na kuona thamani ya mkataba wa mchezaji huyo ni kuona sawa na kiasi hicho,” alisema Ibwe.

Kuna taarifa kuwa Fei Toto ameanza kutajwa katika klabu mbalimbali ikiwamo moja kubwa hapa nchini.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live