Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Fei Toto kachoka kusubiri

Fei Toto Aucho Yanga Kiungo wa Yanga, Feisal Salum (kulia) akiwa na Aucho

Sat, 22 Jan 2022 Chanzo: Mwanaspoti

Baada ya juzi kupasha misuli kwa mechi ya kirafiki dhidi ya Mbuni iliyopo First League, Kiungo wa Yanga, Feisal Salum ‘Fei Toto’ amezidi kukazia kuwa nia yao kuu msimu huu ni kubeba ndoo ya Ligi Kuu Bara.

Yanga ipo kileleni mwa msimamo wa ligi ikiwa na pointi 32, ikicheza mechi 12, ila kupoteza hata moja, ikishinda 10 na kutoka sare mbili ikiiacha Simba iliyo nafasi ya pili kwa tofauti ya alama nane, japo yenyewe ina mchezo mmoja mkononi.

Fei miongoni mwa wachezaji wenye mchango mkubwa wa mafanikio ya Yanga kwa sasa kwa namna anavyocheza akiwa amefunga mabao manne na kuasisti mara mbili katika mechi za ligi hadi sasa na amekazia kuwa nia yao ni kufanya vizuri kila mechi ili kubeba ubingwa ilioukosa kwa misimu minne iliyopita.

“Tunautaka ubingwa, timu iko vizuri pia kila mchezaji anajituma kuhakikisha tunafanya vizuri kwenye kila mechi ili tuweze kufikia malengo yetu,” alisema Feisal na kuongeza;

“Yanga ya sasa viongozi wanajitahidi kututimizia kila kitu kwa ubora na kwa wakati hivyo kazi yetu inabaki kupambana kuhakikisha tunafikia malengo na naamini tutafanya hivyo.”

Sambamba na hilo, kiungo huyo alisema msimu huu amepanga kufunga mabao zaidi ya 15 na juu ya ‘kombinesheni’ yake na viungo wenzake Yannick Bangala, Khalid Aucho na fowadi Fiston Mayele na kusema; Advertisement

“Mimi nacheza maeneo yote ya kiungo kuna kipindi nilicheza namba sita, nane na sasa namba 10 na mara nyingi mwalimu ananisisitiza majukumu yangu ya kwanza ni kuichezesha timu, kutoa asisti na kufunga hivyo kwa kushirikiana na wachezaji wengine tunahakikisha kila tulichoelekezwa na mwalimu kinatimia.”

Yanga kesho itakuwa Uwanja wa Ushirika Moshi kuvaana na Polisi Tanzania iliyopopo nafasi ya nne ikiwa na pointi 18 baada ya mechi 12, ikishinda mara nne, sare sita na kupoteza mbili.

Chanzo: Mwanaspoti