Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Fei Toto azua gumzo Mkutano Mkuu wa Yanga

Fei Toto Sainii.jpeg Fei Toto azua gumzo Mkutano Mkuu wa Yanga

Mon, 26 Jun 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Klabu ya Yanga imetangazo mapata ya mauzo ya wachezaji waliyowapata msimu uliyopita huku mchezaji aliyeuzwa ni kiungo Feisal Salum.

Yanga ilimuuza Feitoto kwa Azam FC kwa dau lililofichwa kwa pande hizo mbili, lakini waliwekeana vipengele ambavyo timu hizo zitaendelea kunufaishana kwa mchezaji huyo.

Akizungumza katika mkutano mkuu wa klabu hiyo Mkurugenzi wa Fedha, Sabri Sadick amesema bajeti ya mapato na matumizi iliyotumika msimu uliopita huku akitaja mapato waliyoyapata kwa upande wa mauzo ya wachezaji ni Sh200 milioni kwa mchezaji Feisal Salum ‘Fei Toto’ kwenda Azam ambapo awali dili lake halikuwekwa wazi.

“Mauzo ya wachezaji ni Sh200 milioni kama mnavyojua tumeweza kumuuza Feisal Salum ‘feitoto” amesema Sabri

Feisal amesaini mkataba wa miaka mitatu, ambao utamfanya akae kwenye timu hiyo ya Chamazi hadi 2026.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: