Kiungo wa Yanga SC, Feisal Salum ‘Feitoto’ ametinga tena kwenye ofisi za Shirikisho la Soka Tanzania TFF akiwa na Mwanasheria aliyemsaidia Saimon Msuva kushinda kesi CAS.
Safari hii amewasilisha barua ya maombi kwa TFF akitaka kuvunja mkataba wake na klabu yake ya Yanga SC.
Yasmin Razak ndiye ambaye alimsaidia Simon Msuva kule Wydad Casablanca na kushinda kesi CAS ambapo klabu yake hiyo iliamriwa kumlipa Msuva Tsh bilioni 1.6.
“Waandishi msikurupuke kwenye kusema Feisal kaonewa ama ameshindwa maneno mengi tuwe na uzalendo, ninaomba tuvute subra kwa mara ya kwanza leo Feisal kaleta ombi lake naimani kama litashughulikiwa nina imani na TFF, chombo pekee kinachoweza kuvunja mkataba wa mchezaji ni TFF,” amesema Yasmin Razack.
Jasmin amewahi kusaidia Wachezaji mbalimbali kwenye migogoro ya kimkataba na Club zao akiwemo Simon Msuva, Wilfred Bony aliyewahi kucheza Man City na Swansea na Emmanuel Eboue aliyewahi kucheza Arsenal.
Fei Toto yupo kwenye mgogoro na Timu yake ya Yanga baada ya kujaribu kuvunja mkataba na klabu yake hiyo licha ya TFF kuamua kuwa bado ni mchezaji halali wa Yanga.