Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Fei Toto atoa neno kukosa kiatu mbele ya Aziz KI

Fei Aziz Ms Fei Toto atoa neno kukosa kiatu mbele ya Aziz KI

Wed, 29 May 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kiungo wa Azam FC, Feisal Salum 'Fei Toto' amempongeza Stephane Aziz Ki kwa kuibuka mfungaji bora akipachika mabao 21 huku akiweka wazi kuwa alistahili.

Fei Toto ambaye amefunga mabao 19 akiachwa mabao mawili na kinara huyo ambaye walikuwa wanakimbizana kwenye ushindani, amesema licha ya kukosa kiatu cha dhahabu msimu huu anafurahi kuipambania timu yake kushiriki Ligi ya Mabingwa Afrika.

"Nampongeza Aziz Ki kwa kufanikiwa kutwaa kiatu cha dhahabu, alistahili kutokana na namna ambavyo amepambana, na mimi pia licha ya kukikosa ninafuraha kuipeleka Azam FC Ligi ya Mabingwa nafasi ambayo ndio ilikuwa katika malengo yetu msimu huu," alisema na kuongeza;

"Haikuwa rahisi, nafurahi mimi pia pamoja na kuipeleka Azam FC kimataifa nilionyesha ushindani kwenye mapambano ya kiatu, bahati haikuwa yangu kwani mchezo wa mwisho pia kafunga na mimi nimefunga lakini amekuwa bora kwasababu yeye kafunga mabao matatu mimi nimefunga moja ambalo lilikuwa muhimu na la faida," amesema.

Aziz Ki amepokea kwa furaha pongezi kutoka kwa Fei Toto akimpa moyo kuwa msimu ujao watafanya kama walivyofanya msimu huu lakini kwa ubora zaidi.

"Msimu ujao tutafanya kama tulivyofanya msimu huu lakini kwa ubora zaidi," amesema na kuongeza;

"Nimefurahia namna ambavyo tulikuwa tunapeana changamoto kuelekea kutwaa kiatu cha ufungaji bora, Fei Toto ni rafiki yangu na huwa tunazungumza na ndio maana amenipongeza lakini nakubali kiwango chake na naheshimu kujituma kwake naamini hili litaendelea msimu ujao," amesema Aziz.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live