Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Fei Toto atasubiri sana kuitwa Taifa Stars - Kiemba

Kiemba X Fei Toto Fei Toto atasubiri sana kuitwa Taifa Stars - Kiemba

Tue, 17 Oct 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Legend wa soka nchini, Amri Kiemba ame-share uzoefu na soka la Tanzania, akisema kuwa mchezaji mzawa akiondoka timu za Kariakoo (Simba au Yanga) ataishi maisha magumu.

Kiemba amesema kuwa, fei Toto baada ya kuondoka Yanga, itachukua muda mrefu sana kuitwa timu ya Taifa ya Tanzania 'Taifa Stars'.

“Hata mimi nilivyoondoka Yanga, miaka mitano sikuitwa timu ya Taifa, niliondoka Yanga 2007, nimekuja kuitwa timu ya Taifa 2011. Nimetoka Yanga nikaenda Miembeni Zanzibar, Moro United wanaitwa wote lakini mimi siitwi.

“Mtu akikukosea unaadhibu nchi nzima, unaweza kuona Fei Toto timu ya Taifa anaisikia tu awe na kiwango au awe hana," amesema Kiemba.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live