Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Fei Toto arudisha makali yake Azam FC

Feisal Leo Fei Toto arudisha makali yake Azam FC

Mon, 6 Nov 2023 Chanzo: Mwanaspoti

Kiungo wa Azam FC, Feisal Salum ‘Fei Toto’ namba zinambeba. Mwanaspoti limefanya uchambuzi licha ya kiungo huyo kucheza dakika chache tangu amejiunga na kikosi hicho.

DAKIKA 593

Fei Toto ametumika katika dakika hizo kwenye mechi nane alizocheza hadi sasa kabla ya mchezo wa jana ambao timu yake ilishuka kumenyana na Ihefu FC ugenini.

Azam FC ilikuwa ugenini kwenye mchezo huo ambao ni wa tisa kwao baada ya kucheza mechi nane wakishinda mitano, kufungwa mbili na kutoka sare moja.

Ndani ya dakika 593, Fei amehusika kwenye mabao sita kati ya 16 yaliyofungwa na timu yake.

ASISTI 2

Licha ya Azam FC kuwa na mawinga wengi wenye kasi lakini kiungo huyo mshambuliaji amehusika kwenye kutoa pasi mbili zilizozaa mabao kwenye mchezo dhidi ya Mashujaa timu yake ikiibuka na ushindi wa mabao 3-0.

Kwenye mechi nane za Azam FC alizocheza kiungo huyo wa zamani wa Yanga, Fei Toto, amefunga mabao manne akitoa asisti (pasi za mabao) mbili.

Kiungo huyo amefunga mabao matatu kwenye mchezo dhiti ya Tabora United timu yake ikiibuka na ushindi wa mabao 4-0, ametoa pasi mbili za mabao kwenye mchezo dhidi ya Mashujaa timu yake ikiibuka na ushindi wa mabao 3-0.

Azam FC jana ilishuka dimbani kuikabili Ihefu FC ikiwa na kumbukumbu nzuri ya matokeo kwenye mchezo wa ugenini baada ya kuiduwaza Mashujaa mabao 3-0 kwenye uwanja wake wa nyumbani.

Mwanaspoti lilimtafuta kiungo huyo kuzungumzia mwendelezo wake mzuri alisema atafanya kwa vitendo haoni sababu ya kuzungumza na wana habari kwa sasa kwani ni mapema sana.

“Ninachokifanya uwanjani kitazungumza sioni sababu ya kuzungumza kila ninapoipambania timu yangu huo ni wajibu wangu na ndio sababu viongozi walinipa mkataba wa kuitumikia Azam FC.” alisema Fei Toto.

Fei alipotea kwa siku za hivi karibuni na kuonekana kunenepa kiasi cha kutochaguliwa Timu ya Taifa ya Tanzania, sasa ameanza kukaa sawa na kurudi kwenye kiwango chake.

Chanzo: Mwanaspoti