Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Fei Toto apewe heshima yake

Nabi Na Fei Toto Fei Toto apewe heshima yake

Mon, 5 Dec 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kiungo mshambuliaji wa Yanga, Feisal Salum 'Fei Toto' kwa sasa anaibeba klabu yake mabegani mwake anajitoa sana, amekua akileta madhara makubwa akiwa katika eneo la 18 ndani/nje mpira wake lazima ulete madhara.

Kiungo huyo Mzaliwa wa Zanzibar mpaka sasa amekua na mchango mkubwa sana kwa upande wa Kikosi cha Yanga Sc.

Ni muda wa kumpa heshima kubwa, kutokana na thamani yake anayoonyesha Uwanjani. Kubwa zaidi ni mchezaji mzawa ambae kuna muda anatoa darasa kwa hawa ma-proo wa Ligi Kuu.

Jana, anaifungia Yanga Sc goli muhimu na la ushindi katika Dakika za Jioni kabisa mbele ya Tanzania Prisons.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live