Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Fei Toto anautaka ufungaji bora NBCPL

Fei Toto Vs Coast Fei Toto

Sun, 8 Oct 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kiungo wa timu ya Azam FC baada ya kufunga bao juzi walipoumana na Caostal Union, ameweka wazi kuwa msimu huu nia yake ni kutwaa kiatu cha ufungaji bora Ligi Kuu Bara.

Fei ameeleza hayo baada ya kufunga bao pekee kwenye mechi hiyo iliyoisha kwa ushindi wa bao 1-0 iliyochezwa Uwanja wa Mkwakwani, Tanga na kuirejesha Azam kileleni mwa msimamo wa ligi hiyo.

Bao hilo limefanya mchezaji huyo kufikisha mabao manne baada ya mechi tano akishika nafasi ya pili nyuma ya Jean Baleke wa Simba anayeongoza kwa mabao matano ambapo leo anatarajiwa kuwa uwanjani kupepetana na Singida Big Stars.

Fei alisema anafahamu si kazi rahisi kufanya hivyo lakini kwa kuwa lengo lake ni kuipambania timu yake basi yuko tayari pia kuendelea kufunga kila anapopata nafasi ili aipiganie timu hiyo na kutimiza ndoto zake.

“Tutegemee nakwenda kuwania kiatu msimu huu maana nipo kwa ajili ya kuipambania timu yangu pamoja na wachezaji wenzangu, siwezi kuzungumza sana kwamba nitafunga mabao mangapi mpaka mwisho lakini ngoja tuone itakuwaje lakini nimepanga kufunga sana msimu huu,” alisema Fei.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live