Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Fei Toto anastahili tuzo

Fei Toto 9 Goals Fei Toto.

Thu, 1 Aug 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kiungo Feisal Salum anaingia kwenye orodha ya nyota waliofanya kazi kubwa kwenye kutimiza majukumu yao ndani ya uwanja akiwa ni chaguo la kwanza la Kocha Mkuu, Bruno Ferry msimu wa 2023/24.

Kwa mujibu wa mchambuzi wa mpira Bongo Mohamed Mohamed maarufu kama Dr Mo amebainisha kuwa kiungo huyo anastahili tuzo yake binafsi kutokana na jitihada kubwa ambazo alifanya ndani ya uwanja katika kutimiza majukumu yake.

“Feisal Salum yupo mmoja na anastahili kupata tuzo yake binafsi ukiweka kando ya ile ya pamoja ambayo pengine anaweza kuitwaa kama uwa kwenye kikosi bora cha msimu ambacho hicho kitatangazwa ukumbini kwani alifanya kazi kuwa.

“Unaona kwenye kufunga, kutoa pasi na Azam FC imemaliza ikiwa nafasi ya pili inashiriki Ligi ya Mabingwa Afrika, Fei alifanya kazi kubwa kwa kushirikiana na wachezaji wengine, hakika anastahili tuzo.”

Ipo wazi kwamba ni mabao 19 alifunga msimu wa 2023/24 akitumia mguu wa kulia kutupia mabao 13 na ule wa kushoto mabao matatu. Ndani ya 18 alifunga mabao 17 nje ya 18 mabao mawili alicheza mechi 29 na kukomba dakika 2,442.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live