Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Fei Toto amvulia kofia Aziz KI

Fei Aziz Ms Fei Toto amvulia kofia Aziz KI

Thu, 30 May 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Baada ya Kiungo wa Azam FC, Feisal Salum Abdallah 'Fei Toto' kukosa kiatu cha ufungaji bora wa Ligi Kuu ya NBC amempongeza mshindani wake Stephan Aziz Ki kwa ubora aliouonesha.

Fei amesema hayo leo wakati Kikosi cha Azam FC kikiondoka Dar es Salaam kuelekea Zanzibar kwa ajili ya fainali ya Kombe la Shirikisho la CRDB ambayo itapigwa Jumapili, Juni 2, 2024 dhidi ya Yanga SC.

"Mimi sina la kuongea zaidi ya kumpongeza, Aziz Ki ni mchezaji mmoja mzuri sana kila mtu anamjua, nampa hongera sana kwa kuwa mfungaji bora na Mwenyezi Mungu aendelee kumfikisha mbali zaidi," amesema Fei Toto.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live