Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Fei Toto amemwacha mbali Mudathir

Fei Toto Mudathri Fei Toto amemwacha mbali Mudathir

Fri, 3 May 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Meneja wa Idara ya Habari na Mawasiliano wa Klabu ya soka ya Azam, Zakaria Thabiti 'Zaka za Kazi' amesema kuwa wanamkosea heshima kiungo mshambuliaji wao, Feisal Salum Abdallah 'Fei Toto' kumfananisha na kiungo wa Yanga, Mudathir Yahya Abbas.

Zaka amesema kuwa Fei Toto ambaye alijiunga na Azam wakati wa dirisha kubwa msimu huu akitokea Yanga, amechangia mabao mengi kwa Azam msimu huu kuliko Mudathir alivyochangia mabao kwa Yanga.

"Feisal Salum kafunga goli 14 kwenye mechi 24, halafu bado kuna mtu alikuwa anamfananisha na Mudathir Yahya," amesema Zaka za Kazi.

Kwa upande wa Mudathir yeye amefunga mabao 8.

Je, unadhani ni sahihi kumfananisha Mudathir na Fei Toto?

Chanzo: www.tanzaniaweb.live