Mchambuzi wa Soka kutoka Clouds FM, Farhan ameibuka na kuzungumzia sakata la mchezaji Feisal Salum na waajiri wake, Yanga Sc baada ya TFF kuamua kuwa mchezaji huyo ni mali ya Yanga.
Binafsi sikuandika tena kuhusu suala la FEISAL, kwakuwa tushaongea sana hakuna kitu kilichosalia ambacho kinapaswa kuandikwa tena.
FIFA waliagiza kipengele cha KUVUNJA MKATABA lakini waliweka vitu ambavyo vifuatwe ili uvunje mkataba wako na klabu kwakuwa walijua watatokea watu watatafsiri tofauti eneo hilo, ukisoma FIFA wanachotaka basi majibu yote unapata.
FIFA wanasema kuvunja mkataba wakati msimu unaendelea (on the course of the season) lazima kuwe na makubaliano ya pande mbili (mutual agreement) na sio Unilateral (pande moja ikiwa na maana klabu au Mchezaji pekee)
Hii ndio sheria hata kama Hakimu atasoma hukumu huku analia kwa uchungu lakini ndio sheria, bahati mbaya sana sheria haioni (Andha Kanoon) sheria ipo kwa ajili ya haki na haki ndio ushindi.
Huenda ni kweli FEISAL anaenda mazoezini na Bodaboda lakini kwenye mkataba kuna sehemu imeandikwa apewe gari? Huenda Feisal anakula ugali na sukari je kuna sehemu kimkataba wanatakiwa wampe chips kuku? Yanga wanacomply na mambo ya KIMKATABA tu ila mengine ni ziada.
FEISAL ataondoka Yanga hiyo haina shida lakini CAS ikitokea wataenda atapigwa faini na adhabu, maisha yataendelea kwakuwa hakuna kitu chochote alichofanya kwa usahihi kwa mujibu wa sheria za mpira.
YANGA hawapambanii kumkomoa Feisal ila wanalinda image yao kama taasisi, restoration of order! Taasisi inalinda maslahi yake tu sio kwamba wana shida sana Feisal.
Watu wa pembeni wawaache YANGA na FEISAL wakae mezani wamalizane kwa amani, kwa ajili ya kipaji cha Feisal na maslahi yake na kwa heshima ya Yanga, naamini ndio busara pekee na ya mwisho Yanga wataifanya kwa Kijana wao waliomtengeneza.
Makofi hayawezi kumkuza mtoto, yatamuumiza.