Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Fei Toto ahama kwao, atimkia ushuani

Feisal Phone.jpeg Fei Toto ahama kwao, atimkia ushuani

Thu, 19 Jan 2023 Chanzo: Mwanaspoti

Hatimaye baada ya usajili kufungwa Jumapili Januari 15 usiku, huku mashabiki wakitafuta kugundua kuwa kiungo Feisal Salum Fei Toto amejiunga na timu gani, mwenyewe anaishi kishua Zanzibar bila presha.

Usajili ulifungwa Jumapili usiku na Fei Toto ambaye ana matatizo na timu yake ya Yanga alikuwa anafikiriwa kuwa anaweza kuwa ameshapata timu ya kujiunga nayo, lakini kwenye majina yote ya usajili hayupo.

Hata kwenye mechi ya Yanga ya juzi dhidi ya Ihefu bado mashabiki walikuwa wanaulizana kama mchezaji huyo ameshapata timu, au Yanga wameamua kumuuza, lakini ukweli ni kwamba Mwanaspoti limechunguza na kugundua kuwa bado yupo zake Zanzibar na sasa akiishi sehemu ya kishua zaidi.

Chanzo cha uhakika ambacho kipo karibu na mchezaji huyo kinasema wakati yote hayo yanaendelea Fei Toto hana habari na kelele za mashabiki wa Yanga ndiyo kwanza yupo nje ya mji huko kwao Zanzibar akiendelea na kufanya mazoezi ya kulinda kiwango chake.

"Ni adimu sana Fei Toto kumuona mjini, zaidi zaidi ni kwenye mazoezi hata nyumbani kwao haishi hapo, anapita kuwasalimia tu, anaishi kwa kificho sana wapo wanaomuona kwenye hoteli kubwa hapa Zanzibar.

"Jambo kubwa analoliamini na msimamo wake anataka kipaji chake kimlipe akiwa kwenye kiwango kwa sababu anajua soka ni la muda mfupi na haonyeshi kama ni mtu wa kurejea Yanga kabisa na wala hataki sana stori hizo. Anaishi sehemu za kishua sana kwa sasa, kwao alishaondoka muda kidogo.

"Anaendeshwa na kwenye magari tofauti tofauti na amekuwa akiishi kwa siri kubwa siku za hivi karibuni, sidhani hata kama anaifutilia Yanga sana kwa sasa naona kama anawaza mambo yake tu," alisema rafiki yake wa karibu sana.

Desemba 24 kiungo huyo aliaga Yanga kupitia barua iliyochapishwa na nyota huyo kupitia mtandao yake ya kijamii aliandika "Umekuwa wakati mzuri sana wa kuichezea Klabu ya Yanga yenye historia kubwa na ya kuvutia nchini na Afrika yote,"

"Tumekuwa na nyakati nyingi mchanganyiko, tulifurahi pamoja pale furaha ilipokuja uelekeo wetu na tulihuzunika pamoja nyakati mbaya zilipotutokea, nitakumbuka mengi mazuri yaliyotokea pamoja na nitasahau yote mabaya kwa haraka sana,"

Wakati Feisal akiaga taarifa iliyotolewa na klabu hiyo iliendelea kusisitiza kwamba nyota huyo bado ni mali yao kwani ana mkataba hadi kufikia Mei 30, 2024 na tayari walianza mazungumzo na wawakilishi wake wakiongozwa na mama yake mzazi ili kuboresha maslahi yake.

Kutokana na sintofahamu hiyo uongozi wa Yanga ulimshtaki mchezahi huyo Kamati ya Sheria na Hadhi za Wachezaji ya Shirikisho la Mpira wa Miguu wa Tanzania (TFF) ambayo imethibitisha kuwa staa huyo bado ni mali ya Yanga kwa mujibu wa mkataba.

Chanzo: Mwanaspoti