Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Fei Toto afunguka aliyoyapitia Azam FC

Fei Hatrick Fei Toto afunguka aliyoyapitia Azam FC

Thu, 28 Sep 2023 Chanzo: Dar24

Kiungo kutoka Visiwani Zanzibar anayekipiga Azam FC, Feisal Salum Abdallah ‘Fei Toto’ amekiri wakati anajiunga na timu hiyo alikuwa na mwili mkubwa, lakini kwa sasa amejitahidi kupambana hadi kukata zaidi ya kilo sita na kujiona mwepesi na kuanza kurejesha makali aliyokuwa nayo enzi akiitumikia Young Africans.

Fei Toto amejiunga na Azam FC msimu huu baada ya kuuzwa kutoka Young Africans aliyoifanyia mgomo tangu mwishoni mwa Desemba mwaka jana kabla ya Rais Samia Suluhu Hassan kuingilia kati kwenye hafla ya kuipongeza timu hiyo ya Jangwani kwa kutinga Fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika msimu uliopita.

Kiungo huyo amesema awali alipojiunga Azam FC alikuwa na uzito wa kilo 75, lakini baada ya kupigishwa tizi la maana kwa sasa amebaki na kilo 69 na kujiona mwepesi na kurejea kwenye ule utamu uliompa mashabiki akiwa na Young Africans aliyoichezea misimu minne.

Fei amesema wakati anaanza kucheza alipata wakati mgumu sana, kwani alikuwa kibonge ila anamshukuru sana kocha kwani alimsaidia mno na kumrejeshea katika hali ya kuwa fiti.

Timu ilinipatia mkufunzi maalum wa kunifundisha mazoezi binafsi yalinisaidia kurudi katika hali yangu, kwani nilikaa nje karibu miezi minne bila kucheza na kwa bahati nimepunguza uzito na sasa nimeanza kurejea katika makali niliyokuwa nayo Young Africans, amesema Fei Toto aliyewahi kuichezea JKU na kutua kwa muda Singida United.

Kiungo huyo alifunga mabao matatu katika mechi ya kwanza wa Ligi Kuu dhidi ya Tabora United iliyokuwa na wachezaji pungufu.

Chanzo: Dar24