Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Fei Toto aandika malengo yake 3 mhimu msimu huu

Feisal Salum Fei Toto Malengo Fei Toto aandika malengo yake 3 mhimu msimu huu

Thu, 27 Oct 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kuna wachezaji wanaocheza eneo la katikati ya uwanja halafu kuna Feisal Salum. Fundi wa mpira kutoka katika visiwa vya karafuu kule Zanzibar. Ni nembo ya ubora wa soka la Tanzania kw sasa.

Jana akitokea benchi, alingia uwanjani na kufunga bao lililoipa Yanga SC ushindi wa bao 1-0 dhidi ya watoza ushuru wa Kinondoni, KMC.

Baada ya mchezo huo, Feisal amepiga stori na YANGA MEDIA na kutaja malengo yake matatu aliyopanga kuyafabikisha msimu huu.

KUISAIDIA YANGA KUTETEA UBINGWA

"Nataka kupambana zaidi msimu huu kuisaidia timu yangu kutetea ubingwa wa Ligi Kuu ya NBC. Naamini mashabiki wetu wana shauku ya kuona tunatetea kombe letu, hivyo jukumu letu wachezaji ni kupambana kuhakikisha tunalitimiza hilo."

GUE KUSHINDA TUZO YA KIUNGO BORA WA MSIMU

"Hii ni ndoto yangu kubwa msimu huu kuhakikisha nafanya vyema na kubeba tuzo ya kiungo bora wa msimu.

"Najua changamoto itakuwa kubwa kutokana na uwezo wa wachezaji wengine wanaocheza nafasi hiyo lakini napambana sana kwenye mazoezi kuhakikisha nabeba tuzo hiyo mwisho wa msimu."

KUFUNGA MABAO 12 MSIMU HUU

"Msimu uliopita nilifunga mabao 6 lakini msimu huu nimeweka malengo ya kufunga mabao 12. Ni ngumu lakini naamini inawezekana.

"Mpaka sasa nimefunga mabao manne lakini kwa ushirikiano ninaoupata kwa wenzangu nina uwezo wa kufunga mabao 12 msimu huu."

Chanzo: www.tanzaniaweb.live