Kiungo wa Azam FC, Feisal Salum ‘Fei Toto’ amesema amezungumza na wachezaji wenzake kikosini hapo na kukubaliana kufikia malengo yao msimu ujao wa 2023/24 ikiwa ni pamoja na kupata ushindi kwenye mechi zao.
Fei Toto amesajiliwa na Azam FC akitokea Yanga, ataanza changamoto mpya kwenye kikosi hicho msimu wa 2023/24.
Timu hiyo ambayo itakuwa chini ya Kocha Mkuu, Youssouph Dabo raia wa Senegal na msaidizi wake, Mfaransa, Bruno Ferry wameanza maandalizi ya msimu wa 2023/24, jana Jumapili ilieleka jijini Sousse nchini Tunisia kwa ajili ya kambi ambayo itaanza Julai 9 hadi 30, 2023.
Akizungumza nasi, kiungo huyo amesema: “Tupo na wachezaji wengine ambao ni wapya kwenye kikosi, tumezungumza kwa pamoja kuona namna gani tunafikia malengo ambayo tunahitaji kuyafikia, tutapambana kufanya vizuri.”