Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Fei Toto: Niliugua tumbo kabla ya kuwavaa KMC

Fei Toto Mashuti Fei Toto na Aziz Ki

Thu, 27 Oct 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mfungaji wa goli pekee la Yanga katika mchezo wa jana dhidi ya KMC, Feisal Salum 'Fei Toto' amefichua siri ya kilichomuwezesha kuipa Yanga ushindi kwenye mchezo huo.

Akizungumza mara baada ya mchezo huo kumalizika katika Dimba la Mkapa kwa Yanga kuibuka na ushindi wa bao 1-0, Feisal aliyefunga bao hilo dakika ya 80 amesema;

"Nilipata hitilafu kidogo tumbo lilikuwa linanisumbua ndiyo maana sikuanza leo (jana) katika kikosi cha kwanza kwa hiyo nikaanzia nje ili kuona hali yangu kama itakaa sawa.

"Kilichonisaidia kuipa Yanga ushindi nimefuata maelekezo ya mwalimu ambayo alinipatia kabla ya kuingia uwanjani.

"Unajua tumetoka dabi (Simba na Yanga) ni mechi kubwa, kulikuwa na uchovu kwa hiyo mwalimu akaamua kupumzisha baadhi ya wachezaji na wengine walikuwa na majeruhi, wengine hawakuwa fiti, lakini tunamshukuru Mungu tumepata ushindi," amesema Fei Toto.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live