Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Fei Toto: Mashabiki tuombeeni, tutawapiga Waarabu leo

Feisal Salum Fei Toto Fei Toto na Mayele

Wed, 9 Nov 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Unaambiwa ugumu wa mchezo wa marudiano wa Kombe la Shirikisho Afrika, kati ya Yanga na Club Africain ya Tunisia, umemfanya Nahodha Msaidizi wa Yanga, Feisal Salum ‘Fei Toto, kuomba msaada wa maombi kwa mashabiki wa klabu hiyo ili wapate ushindi.

Yanga ambayo imeweka kambi yake katika Hoteli ya Golden Tulip Carthage nchini Tunisia, leo majira ya saa 2:00 usiku inatarajiwa kuingia Uwanja wa Olympique Hamadi Agrebi kucheza na wenyeji wao Club Africain katika mchezo wa marudiano wa Kombe la Shirikisho baada ya ule wa awali uliopigwa Uwanja wa Mkapa, Dar kumalizika kwa suluhu.

Fei Toto alisema kwa upande wao kama wachezaji wanaijua presha kubwa inayowakabili lakini watapambana kuwapa furaha mashabiki wao ila jukumu lao kama mashabiki kwa sasa ni kuwaombea dua ili wafanikishe mipango yao kwa usalama.

“Kwa niaba ya wachezaji wenzangu ninawaomba mashabiki wote wa Yanga kuendelea kutuombea kwani sisi kama wachezaji tupo tayari kupambana kwa ajili ya kuwapa furaha pamoja na kuwa presha ya mchezo huu ni kubwa.

“Natambua kuwa tuna deni kubwa sana kwa Watanzania na mashabiki wote, hivyo nasi tutapambana sana ili kuona timu ikicheza hatua ya makundi, hivyo tunaomba maombi pekee kutoka kwao,” alisema Fei Toto.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live