Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Fedha za CAF Super League zaipa jeuri Simba SC

Image 709 1024x640.png Fedha za CAF Super League zaipa jeuri Simba SC

Wed, 24 May 2023 Chanzo: Dar24

Shilingi Bilioni 5 zitakazotolewa na Shirikisho la Soka BArani Afrika ‘CAF’ kwa ajili ya maandalizi ya michuano ya Super League, zimeipa jeuri Simba SC kuimarisha kikosi chao kuelekea msimu ujao 2023/24.

Simba SC imedhamiria kufanya usajili mkubwa, baada ya timu yao kumaliza msimu wa pili mfululizo pasina kutwaa taji lolote la ndani nan je ya Tanzania, halia bayo imezua taharuki kwa Mashabiki na Wanachama, huku baadhi yao wakiutupia lawama Uongozi wa klabu hiyo.

Mbali na fedha hizo, Simba SC itavuna fedha nyingine kutoka CAF kama zawadi ya kufika hatua ya Robo Fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika msimu huu kiasi cha Dola za Marekani 900,000 (zaidi ya Sh. bilioni 2.1).

Kwa mujibu wa habari kutoka ndani ya klabu hiyo, zinasema uongozi wa timu hiyo utatumia sehemu kubwa ya fedha kufanya usajili, huku klabu hiyo ikianza kuhusishwa na majina ya nyota mbalimbali wa ndani na nje ya Tanzania.

Moja ya majina ya wachezaji wa ndani wanaohusishwa kujiunga na Simba SC ni kiungo nyota wa Azam FC, Sospeter Bajana.

Bajana amehusishwa kujiunga na Simba SC baada ya mkataba wake na Azam FC kufikia ukingoni huku ikidaiwa kuwa hajaongeza mkataba na waajiri wake hao ambao wako katika mazungumzo.

Meneja wa Habari na Mawasiliano wa Simba SC, Ahmed Ally, amesema uongozi wa timu hiyo unaendesha mchakato wao wa usajili kwa umakini mkubwa.

“Bado hatujaweka wazi wachezaji tunaowataka ingawa yapo majina ya wachezaji tunaowataka, uongozi upo makini kufanya usajili wa nguvu kwa sababu fedha zipo,” amesema Ahmed na kuongezea,

“Tuna mzigo mkubwa ukiunganisha fedha za mwekezaji wetu, Mohammed Dewji, fedha za Super League na vyanzo vingine, hilitatufanya kuwa na jeuri ya kufanya usajili kwa wachezaji tunaowataka,” amesema

Chanzo: Dar24
Related Articles: