Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Faridi Mussa aongeza kandarasi Yanga, atamwachia jezi Chama?

Chama Farid Gn Faridi Mussa aongeza kandarasi Yanga, atamwachia jezi Chama?

Tue, 2 Jul 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Klabu ya Yanga SC imetangaza kumuongezea mkataba wa miaka miwili Nyota wa Kitanzania Farid Mussa Malick utakaomalizika mwaka 2026.

Nyota huyo ni moja ya nyota waandamizi wa klabu hiyo ambapo ameichezea toka mwaka 2020.

Farid Mussa ni winga anayeweza kucheza nafasi ya kiungo pia, alisajiliwa na Yanga baada ya janga la Corona kuharibu mipango yake ya kurudi Hispania kucheza soka la kulipwa.

Awali alikuwa akihitajika zaidi na Simba kabla ya kusajiliwa Yanga, lakini moja ya kikwazo alikuwa ni Kiungo Clatous Chama ambaye alikuwa anacheza eneo hilo hilo na alikuwa wa moto sana.

Hali hiyo ilimfanya mchezaji huyo kukimbilia Yanga ambako alifanikiwa kutwaa mataji ya Ligi Kuu Matatu, Ngao ya Jamii mara 2, na Kombe la Shirikisho FA mara 3, wakati huo huo akiisaidia timu hiyo kucheza fainali ya kombe la Shirikisho Afrika na kuvaa medali, huku akifikisha timu yake hatua ya robo fainali Ligi ya Mabingwa Afrika msimu uliopita.

Akizungumzia sakata lake la kutosaini Simba na Kujiunga na Yanga Farid Mussa alisema alikuwa anamuwazia sana Chama kumnyang’anya namba pale Msimazi, ndipo akapata akili ya kujiunga namba.

Alipofika Yanga alikabidhiwa jezi namba 17 sawa na ile anayovaa Clatous Chama pale mitaa ya msimbazi, lakini kwa sasa wapo timumoja.

Je Farid Mussa kumuachia Chama jezi namba 17? Endelea kuwa karibu nasi kwa habari za uhakika zaidi.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: