Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Farid Mussa ni wakati wa kuamka usingizini

Faridi Gamondi Farid Mussa ni wakati wa kuamka usingizini

Wed, 24 Apr 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Farid Musa....Akipata timu inayocheza kwa kutumia mawinga asilia au inverted winger bado ana uwezo mkubwa sana.

Kinachomuweka kwenye benchi pale Yanga sio ubora wake kushuka bali ni style of play anayotaka Gamondi timu icheze na namna Yanga ilivyojengwa kwa sajili zake.

Kwa namna hiyo, sio rahisi kumuona Nkane, Okrah na mawinga wengine wakipata nafasi ya kucheza dakika nyingi.

Farid Musa ana uwezo wa kucheza kama winga na hapo hapo amewahi kucheza kama Mlinzi wa kushoto.

Maana yake ni winga wa kisasa anaefit kwenye sayansi ya Mpira ambayo inataka winga mwenye balance ya kushambulia na kuzuia kwenye moment zote timu ikiwa na Mpira na wakati Timu haina mpira.

Farid namuona akienda Simba anaweza kupata nafasi Kikosi cha kwanza na akafanya vizuri zaidi kutokana na mfumo wao na pengine jina lake likaimbwa tena kama Mudathir,Mkude walioonekana kuchoka ila walipoenda timu yenye mahitaji wanayofit wamefanya vizuri nyakati muhimu.

Farid akipata dakika nyingi za kucheza hakuna Kocha wa Timu ya Taifa atamuacha..

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: