Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Farid Mussa afanyiwa upasuaji

Dsa Faridi Farid Mussa afanyiwa upasuaji

Mon, 9 Sep 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Farid Mussa, mchezaji wa Young Africans SC atakuwa nje ya uwanja kwa kipindi cha miezi mitatu baada ya kufanyiwa upasuaji wa majeraha ya misuli ya nyuma ya goti.

Makamu wa Rais wa klabu hiyo, Arafat Haji, amemtembelea Farid jana hospitalini ambapo alionyesha mshikamano na kutoa pole kwa mchezaji huyo.

Arafat alisema, “Tuna matumaini kwamba Farid atapona haraka na kurejea uwanjani kwa nguvu mpya. Timu yetu inahitaji mchango wake mkubwa, na tutamsaidia kwa kila njia.”

Farid ambaye alipatwa na majeraha hayo wakati wa mazoezi, sasa atahitaji muda wa miezi mitatu ili kupona na kuimarisha afya yake kabla ya kurejea kwenye majukumu ya uwanjani. Klabu ya Yanga imethibitisha kwamba itatoa msaada wote muhimu kwa Farid katika kipindi hiki.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live