Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Farid: Gamondi anataka ushindi kila mechi

Faridi Gamondi Farid: Gamondi anataka ushindi kila mechi

Tue, 12 Mar 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kiungo mshambuliaji wa Yanga, Farid Musa amesema kuwa kocha wao, Angel Miguel gamondi anataka kila mchezo washinde na kupata alama tatu hivyo wana wakati mgumu wa kuhakikisha wanapambana li kutimiza maagizo ya mwalimu.

Farid amesema hayo jana baada ya kumalizika mchezo wao dhidi ya Ihefu FC ambapo yanga iliibuka na ushindi wa bao 5-0 katika Dimba la Azam Complex, Chamazi.

“Mechi ilikuwa ngumu lakini mwalimu anataka alama tatu kila mchezo. Gamondi anataka kila mechi tushinde na tupate alama tatu muhimu.

“Mimi sikuwahi na wasiwasi sana kuhusu Ihefu kwa sababu uwanja huu kwetu ni machinjio, ni kama uwanja wetu. Mechi ilikuwa nzuri na tunamshukuru Mungu tulipata alama tatu,” amesema Farid Musa.

Mechi ambazo Yanga amefunga mabao matno msimu huu;

◉ Yanga 5 - 0 KMC ◉ Yanga 5 - 0 JKT Tanzania ◉ Yanga 5 - 1 ASAS ◉ Yanga 5 - 1 Simba SC ◉ Yanga 5 - 0 Jamhuri ◉ Yanga 5 - 1 Hausing FC ◉ Yanga 5 - 0 Polisi Tanzania ◉ Yanga 5 - 0 Ihefu FC.

Mechi inayofuata ni Yanga dhidi ya Geita Gold FC.

Pengine Miguel Gamondi ndiye kocha katili zaidi kwenye historia ya Yanga SC?

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: