Baada ya kushambuliwa na walio wengi kwa kupoteza nafasi kadhaa katika mchezo waliopoteza ugenini dhidi ya Horoya, Baadhi ya wachambuzi wameonekana kutomlaumu John Bocco na kusema uimara wa mlinda mlango wa Horoya katika kujilinda unapaswa uzingatiwe.
Akizungumzia mchezo na nafasi alizoshindwa kuzalisha mabao John Bocco Farhan anasema;
" Bocco katika zile nafasi alizopata hakuweza kuzifanya kuwa mabao (magoli) , kama Mshambuliaji anashindwa kutumia nafasi cha kwanza ni kusifia safu ya ulinzi ya Mpinzani"
" Washambuliaji wanasema Kipa akitoka goli linapungua na kama ulivyoona Kipa akiona hana uwezo wa kuokoa alikuwa anatoka anabana mwamba mmoja kama kubashiri (bet) namna ambavyo Bocco atafanya"
"Cha kwanza kwangu ni safu ya ulinzi ya Horoya , cha pili Bocco jana hakuwa katika kiwango tulichokuwa tunategemea kwa sababu ni Mchezaji ambaye amefunga mabao mengi, amefanya mambo mengi makubwa "