Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Farhan: Feisal ni pengo la kimfumo Yanga

Feisal Salum Fei Toto'' Feisal Salum

Mon, 13 Feb 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Wakati Yanga ikianza kampeni za Michuano ya Kimataifa pasipo kiungo wake mahiri Feisal Salum, wengi wameoneshwa kushtushwa na hali hiyo huku wakionekana kukata tamaa hasa bada ya kupata matokeo wasiyoyatarajia mbele ya US Monastr.

Sasa mchambuzi wa Soka, Farhan Kihamu amatolea ufafanuzi nafasi ya Feisal pengo la Feisal katika Kikosi cha Yanga.

"Kocha Nabi aliitengeneza Timu kupitia Feisal kwenye eneo la Kiungo, hata Mwinyi Zahera wakati yupo Yanga aliitengeneza Timu kupitia kwa Feisal na unakumbuka ndiye aliyemshusha chini acheze namba 6 ni kwa sababu Feisal ana-vission (maono) kubwa ya mchezo , umri mdogo wa maana passion (Kiu ya maafanikio) kubwa , anauwezo na ubunifu wa kufanya vitu vyote ambavyo unahitaji Kiungo afanye"

"Nabi alivyokuja hakuwa na kitu kipya zaidi ya kusema Timu itacheza lakini itaunganishwa kupitia kwa Feisal Salum, kwa sababu ni Mchezaji mwenye uwezo, hapati majeraha mara kwa mara kwa hiyo ni mradi wa muda mrefu kwa Yanga"

"Feisal anakupa kitu cha tofauti na Viungo wengine kwa sababu Feisal anapiga pasi za mbele , anapiga mashuti vyote hivi Feisal anafanya , Sasa Feisal ametoka ghafla kwenye mipango, wanapata shida sio kwamba Feisal ni bora sana kuzidi waliopo, Feisal ni pengo lakini si pengo la kwamba Feisal yeye ni pengo la kimfumo

Chanzo: www.tanzaniaweb.live