Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Familia ya soka yamlilia Pele

Pele Rambi Rambi Familia ya soka yamlilia Pele

Fri, 30 Dec 2022 Chanzo: Mwanaspoti

Nguli wa soka Pele amefariki dunia akiwa na umri wa miaka 82, mastaa wa soka dunia wamemlilia mkongwe huyo aliyewahi kutikikisa enzi za ujana wake.

Pele alifarikia hospitali alipokuwa akifanyiwa matibabu tangu alipolazwa jijini Saolo Paolo, Brazil. Pele alikuwa akisumbuliwa na maradhi ya kansa.

Mastaa wa soka duniani wameandika ujumbe kupitia akaunti zao Instagram na Twitter, wakionyesha jinsi ganni wameguswa a kifo cha mkongwe huyo aliywahi kujipatia umaarufu kutokana na kipaji chake cha soka.

Jina lake la utani alikuwa anaitwa 'mfalme', amebeba makombe matatu ya Kombe la Brazil akiwa na kikosi cha Brazil miaka ya 1958, na 1970.

Pele amefunga jumla ya mabao 1,279 katika mechi 1,363 games, alizocheza zikijumuishwa na mechi za kirafiki na kuweka rekodi ya dunia zinazoandaliwa na kampuni ya Guinness.

Mastaa wamlilia Pele na wameandika ujumbe tofauti wakionyesha kuguswa na kifo chake kupitia akaunti zao za Twitter na Instagram.

Wakongwe waongoza maombelezo

David Beckham Mkongwe wa soka aliyewahi kukipiga Manchester United na Real Madrid aliandika "Asante 'Pele' hakika alikuwa na kipaji cha kucheza soka", naye Ronaldo de Lima, Rorbeto Carlos, Gary Lineker, Sir Geoff Hurst, miongoni waliondika ujumbe kuhusu kifo cha Pele.

Cristiano Ronaldo na Lionel Messi waguswa

Nyota wa kimataifa Ureno aliandika ujumbe kupitia akaunti yake ya Instagram “Pole Brazil na familia nzima ya Mr. Edson Arantes do Nascimento, Alipendwa na alikuwa mfano wa kuigwa na mamilioni ya watu, atakumbukwa leo, kesho na milele," kwa upande wa Lionel Messi Bingwa wa Kombe la Dunia Qatar, Messi aliandika ujumbe mfupi tu "Lala kwa amani Pepe'"

Mastaa wa EPL wamlilia Pele Mastaa wanaokipiga Ligi Kuu England wameguswa na kifo cha Pele kwa kuandika ujumbe wakimkumbuka mambo yake mazuri aliyofanya. Mastaa hao ni Marcus Rashford, Harry Kane, Antony, Jesse Lingard, na Gabriel Jesus, Lisandro Martinez, Erling Haaland, Phillipe Coutinho

Mastaa wa kimataifa Brazil waombeleza

Neymar, Antony, Dani Alves, Thiago Silva, Rodrygo, Vinicius Jr, mkongwe Ronaldo de Lima, David Luis na wengine wengi wameomboleza kifo cha Pele kwasababi ndiye aliyetambulisha soka katika taifa na wataendelea kumkumbuka maisha yao yote ya soka, timu ya taifa ya Brazil ilimuombea Pele apone haraka baada ya kulazwa kipindi cha fainali za Kombe la Dunia Qatar.

Klabu zaomboleza

Klabu tofauti kama Manchester United, Real Madrid, Barcelona, Arsenal, Manchester City, AC Milan, Liverpool, Chelsea, na nyingine kibao zimeomboleza kifo cha mkongwe Pele.

Chanzo: Mwanaspoti