Familia ya Malcom X inapanga kuwashtaki FBI,CIA na Polisi wa New York (NYPD) kuhusiana na mauaji ya mwanaharakati huyo yaliyotokea miaka 58 iliyopita.
Familia hiyo inataka fidia ya dola za Kimarekani milioni 100.
Binti wa Malcom X Bi.Ilyasah Shabazz ameyatuhumu mashirika kadhaa ya Serikali ya Marekani kwa kuficha ushahidi kwa njia ya udanganyifu huku akisema "mlikula njama na kutekeleza mpango wenu wa kumuua Malcom X".
"Kwa miaka mingi sasa familia yetu imekuwa ikipigana ili ukweli kuhusiana na mauaji yake uwe wazi".
Malcom X alipigwa risasi tarehe 21 Februari 1965 huko Manhattan.
Baada ya mauaji hayo washirika kadhaa wa mwanaharakati huyo walisema wanaamini mashirika kadhaa ya Serikali yalikuwa yakiufahamu mpango ule na yaliuruhusu utokee.