Baada ya siku kadhaa matajiri Sir Jim Ratcliffe na Sheikh Jassim bin Hamad Al Thani kujitokeza kutaka kuinunua Manchester United, wamiliki wa klabu hiyo, Familia ya Glazer wameibuka na kusema hawapo tayari kuiuza.
Wiki iliyopita, Ratcliffe na Sheikh Jassim waliwasilisha ofa kwa ajili ya kuinunua klabu hiyo, baada ya Glazers kutaka kuiuza. Mchakato wa kuanza kupitia ofa za matajiri hao unatarajiwa kuanza kufanyiwa kazi wiki hii.
Jassim na Ratcliffe wanataka umiliki wa klabu hiyo kwa asilimia 70 mbele ya Familia ya Glazer. Awali bei ya kuiuza Man United ilitajwa na Glazers kuwa ni pauni 5 bilioni (Tsh trilioni 14.13), huku wao wakiwa na madeni ya pauni 680m, huku Sheikh Jassim ambaye yupo Raine Group, alikuwa tayari kulipa madeni hayo.
Taarifa zinaeleza kuwa, Familia ya Glazer haipo tayari kuiuza Man United kwa bei ambayo walikuwa wametaja awali na wanataka bei ipande, kama itashindikana, hawataiuza.
Kutokana na hali ilivyo, huenda Ratcliffe na Sheikh Jassim wakaongeza ofa zaidi ndani ya dili hilo ingawa Glazer wamekuwa na hofu kuwa huenda wakawa hawana uwezo tena wa kuikontroo klabu hiyo.