Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Familia ya Di Maria yatishiwa kuuawa

Sfdgg Familia ya Di Maria yatishiwa kuuawa

Wed, 27 Mar 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Familia ya mshambuliaji wa klabu ya Benfica na timu ya taifa Argentina, Di Maria, imetishiwa kuuawa mara baada ya mchezaji huyo kutangaza anataka kurudi katika klabu yake ya utotoni Rosario Central.

Di Maria alianza kucheza soka katika klabu ya Rosario Central kabla ya kutimkia Benfica ambapo alicheza mechi 125 ndani ya miaka mitatu.

Kisha aliondoka Ureno na kujiunga na miamba ya Uhispania, Real Madrid kabla ya baadaye kuhamia Manchester United, PSG, Juventus na kisha kurejea Benfica kwa sasa.

Mchezaji huyo amesema, anatamani kumaliza soka lake katika klabu hiyo iliyomtoa, hivyo baada ya kauli hiyo familia yake imetumiwa ujumbe wa vitisho vya kuuawa mmoja kati ya wanafamilia wakidai mchezaji huyo hatakiwi kurudi.

Rosario ni jiji kubwa zaidi katika jimbo la kati la Santa Fe, linatajwa kuwa kitovu cha biashara ya dawa za kulevya na uhalifu.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live