Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Fainali ya kisasi Mamelodi, Wydad

Wydad Vs Mamelodi Kisasi Fainali ya kisasi Mamelodi, Wydad

Thu, 2 Nov 2023 Chanzo: Mwananchi

Klabu ya Mamelodi Sundowns imetinga fainali ya African Football League baada ya kuiondosha Al Ahly kwa jumla ya bao 1-0 mechi iliyochezwa Uwanja wa Al Salam jijini Cairo, Misri.

Mchezo wa kwanza uliochezwa Uwanja Loftus Versfeld nchini Afrika Kusini Oktoba 29, 2023 Mamelodi iliibuka na ushindi wa bao 1-0 kabla ya mchezo wa leo uliomalizika kwa sare ya 0-0.

Mamelodi itacheza fainali ya AFL dhidi ya mbabe wake katika nusu fainali ya Ligi ya Mabingwa msimu uliopita Wydad Casablanca ya Morocco iliyomuondosha katika mashindano hayo kwa mabao ya ugenini.

Wydad imetinga hatua hiyo baada ya kuiondosha ES Tunis ya Tunisia kwa mikwaju ya penalti 5-4 baada ya mechi kumalizika kwa sare ya 1-1.

Fainali ya AFL baina ya Mamelodi na Wydad itachezwa Novemba 5, mwaka huu katika dimba Mohamed V nchini Morocco.

Chanzo: Mwananchi